Deuteronomy 12:2-5

2 aHaribuni kabisa kila mahali pao pa kuabudia kwenye milima mirefu, vilima na chini ya kila mti mkubwa ambamo mataifa haya mnayokwenda kuchukua ardhi yao huabudia miungu yao. 3 bBomoeni madhabahu zao, vunjeni yale mawe wanayoabudu, chomeni moto nguzo zao za Ashera; katilieni mbali sanamu za miungu yao na mfute majina yao mahali hapo.

4 cKamwe msimwabudu Bwana Mwenyezi Mungu wenu kama wanavyoabudu wao. 5 dBali mtatafuta mahali Bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda;
Copyright information for SwhKC